Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika muendelezo wa vitisho vya kifedhuli vilivyo tolewa na Raisi wa marekani kumuelekea Kiongozi mkuu wa mapinduzi (mola amuhifadhi), Jumuiya wa walimu wa hawza (Jaamit-mudarisin) Qum, imetoa maelezo ya kupinga vitisho hivi, matini ya maelezo hayo ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
«وإِذْ یَمْکُرُ بِکَ الَّذِینَ کَفَرُوا لِیُثْبِتُوکَ أَوْ یَقْتُلُوکَ أَوْ یُخْرِجُوکَ وَ یَمْکُرُونَ وَ یَمْکُرُ اللَّهُ وَ اللَّهُ خَیْرُ الْمَاکِرِینَ.»
Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe, wakapanga mipango yao, na mwenyezimungu akapanga yake, na Mwenyezimungu ndie mbora wa mipango. (Anfali aya 30)
Mazungumzo ya kishetani na kikhabithi yaliyotolewa na Raisi wa marekani, yakilenga kumtishia Kiongozi wa mapinduzi (Mola amuhifadhi) kwa mara nyengine tena yameonesha ujinga na kiburi cha hali ya juu, Ni wangapi wahalifu waliokuwa na kiburi na majivuno, lakini baadaye walidhalilika na kuwa wadogo; baada ya kujigamba na kujiona wapo juu, waliishia kuwa watu duni na wa kudharauliwa huku wakinaswa katika mtego waliouandaa wenyewe."
Katika tukio la kuhama Mtume (saw) makafiri walifanya kila namna ili kumuuwa Mtume (sawa) lakini matakwa ya Mwenyezimugu hila zao yaliziyeyusha na wakashindwa kukabiliana na nguvu za daima za mwenyezimungu
Hawza Pamoja na uma wa kiislamu inakemea vikali udhalilishaji wa kifedhuli uliofanywa na Raisi asie na aibu wa Marekani
Pasi na shaka aina yeyote ya kuivunjia heshima nafasi ya kiongozi wa mapinduzi (Mola amuhifadhi) kutaleta tija mbaya na hakuna atakaye weza kukabiliana nayo, hizi porojo na mabepari na Mazayuni zinaonesha udhaifu wao, ukweli ni kwamba Kiongozi wa mapinduzi hawezi kutishika na vitisho hivi, na Maisha yake yapo kwenye matarajio ya Mwenyezimungu na maelekezo ya Imamu wa zama (aj)
Maraaji wa dini ndio washika bendra ya kuwaongoa watu na kuwakushanya waislamu katika siasa zinazo endana na utamaduni wa kiislamu, Hadhrat Ayatollah – Udhama Khamenei ni Kiongozi wa mambo yanayo husiana na Mwenyezmungu ukiachilia mbali mambyo ya kiulimwengu.
Aina yeyote ile ya vitisho na kuivunjia heshima nafasi ya Marjiat ni sawa sawa na kutangaza vita na uma wote wa kiislamu, na sawa na kuwasha moto ambao miale yake itaenea sehemu zote
«وَسَیَعْلَمُ الَّذِینَ ظَلَمُوا أَیَّ مُنْقَلَبٍ یَنْقَلِبُونَ.»
Na wano dhulumu watakuja jua ni mgeuko gani watakao geuka.
Jumuiya ya walimu wa hawza Qum
Shura ya juu ya hawza
Kituo cha uongozi wa hawza
Maoni yako